Kamati ya siasa mkoa wa pwani yaendeleza ukagizi wa miradi kwa kishindo


Leo tarehe *18/11/2023* Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Pwani chini ya Mwenyekiti wake ndugu *Mwinshehe Mlao* imeendelea na ziara yake ya ukaguzi wa Miradi ya maendeleo katika Wilaya za Kisarawe na Mkuranga na kujionea Utekelezaji mkubwa wa Ilani ya uchaguzi ya CCM *2020 -* *2025.*

Kamati hiyo imekagua jumla ya miradi mikubwa  mitano ya Sekta ya elimu na afya na kuridhishwa na Utekelezaji wa Ilani kwa vitendo.



Akisoma taarifa ya ujenzi wa jengo la huduma za dharura katika Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe mchumi wa Halmashauri hiyo *ndugu Deogratius* *Lukomanya* amesema walipokea jumla ya shilingi *milioni 300* kwa ajili ya kuboresha huduma za dharura kwa wagonjwa.

Jengo hilo limekuwa likihudumia wateja kati ya 4 - 6 kwa siku na linahudumia wateja kati ya 120 - 180 kwa Mwezi.

Kukamilika kwa jengo hilo kumeboresha utoaji wa huduma za dharura kwa wataalamu wa afya kuwa mwepesi kutokana na Miundo Mbinu ya jengo.





Pia jengo hilo la dharura litapunguza msongamano wa wagonjwa kwenye wodi na kutoa huduma sahihi kwa wakati sahihi.

Kwa upande wa Sekta ya elimu Kamati hiyo ilikagua maendeleo ya ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Kitanga iliyopo Kata ya Msimbu Wilayani Kisarawe.

Lengo la mradi huo ni kupunguza umbali wa wanafunzi wa vitongoji vitatu na maeneo ya jirani kwenda kupata elimu katika Shule ya Sekondari Msimbu iliyopo umbali wa zaidi ya *Kilomita 16* ambapo utakapokamilika utahudimia wanafunzi *320* wakiwemo kidato cha kwanza wa mwaka *2024* na waliokuwa wakisoma Msimbu Sekondari watahamishiwa shuleni hapo.




Kuwepo kwa shule hiyo kutapunguza mdondoko wa wanafunzi wa kike waliokuwa wanaacha shule kutokana na kupata ujauzito kwa sababu mbalimbali.

Mradi huo unagharimu zaidi ya shilingi *milioni* *528* , hadi sasa umekamilika kwa *asilimia* *98* na unatarajiwa kukabidhiwa tarehe *30 Novemba* *2023.* 

Katika Wilaya ya *Mkuranga* Kamati ya Siasa Mkoa wa Pwani ilikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa shule ya Msingi Juhudi iliyopo katika Kijiji cha Kipara mpakani Kata ya Mwandege na kujionea vyumba 14 vya madarasa ambavyo vimekamilika na wanafunzi wanavitumia.

Pia walikagua madarasa maalumu ya awali mawili yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 60. Hivyo kufanya jumla ya shilingi *milioni 475,300,000* kutumika katika mradi huo wa BOOST.

Aidha Kamati hiyo ilikagua mradi wa ujenzi wa kituo cha afya cha Nyamato ambacho kinajengwa kwa fedha za mapato ya ndani na nguvu za wananchi na zaidi ya shilingi *milioni* *438* zitagharimu kukamilika kwake.

Hata hivyo Kamati hiyo ilimalizia kukagua mradi wa ujenzi wa shule Sekondari Kilimahewa iliyopo katika Kijiji cha Kilamahewa Kaskazini katika Kata ya Kimanzichana, Tarafa ya Mkamba huku ujenzi huo ukifikia asilimia 94 na unatarajia kugharimu jumla ya shilingi *milioni* *528* hadi kukamilika kwake kwa madarasa 8, matundu ya vyoo 8, Maabara 3, jengo la Utawala, jengo la Maktaba, Chumba cha Tehama na chumba maalumu cha Wasichana.

Awali Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga *Bi Khadija* *Nasir Ally* kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani NDG Mwinshehe Mlao alisema amepokea taarifa ya kuanza kwa ujenzi wa upanuzi wa barabara nne kuanzia Mbagala mpaka Vikundu ambayo itakuwa na Km. 8 na inatarajiwa kuanza ujenzi wake 2024 mwezi Machi.

Amesema upanuzi wa barabara hiyo utachochea shughuli za kiuchumi na usalama utaimarika lakini pia tayari hazina imeshahidhinisha fedha kwa ajili kuwalipa wananchi fidia na zoezi hilo linatarajiwa kuanza tarehe *26/12/2023* kwa wale ambao watapitiwa na mradi huo.

Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani *NDG Mwinshehe Mlao* amesema kilio chake kikubwa ni kuona Wazazi wakiwasomesha watoto waoaana Mhe, Raisi amewaheshisha Wazazi Mkoa wa Pwani kwa kuwajengea Miundo Mbinu bora ya elimu.

Amesema hakuna sababu ya Chama Cha Mapinduzi kushindwa kwenye chaguzi za Serikali za Mitaa, vitongoji na vijiji na uchaguzi Mkuu 2025. Pia amewatahadharisha wanaccm atakayesababisha kushindwa kwa CCM atakufa naye.

Sababu zinazopelekea Mwenyekiti huyo kusema hivyo ni kutokana na utekelezaji mkubwa wa miradi ya maendeleo uliofanywa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe, Dk. Samia Suluhu Hassan Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha amewataka Viongozi hao kumaliza migogoro na tofauti zao kabla ya kumalizika kwa mwaka 2023 ili kuwa wamoja na kufanikisha chaguzi za mwaka 2024 na 2025.

Hata hivyo amemtaka kila Kiongozi aitendee haki nafasi aliyopewa katika kuwahudumia wananchi badala ya kuitumia nafasi hiyo kwa maslahi yake binafsi.

Amewasisitiza kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kumsaidia Mhe. Raisi Samia Suluhu Hassan na wala wasi

kubali kuharibiwa kazi zao na watu waliokata tamaa.

Alihitimisha hotuba yake  kwa kumpongeza Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga kwa ukusanyaji wa mapato na usimamizi mzuri wa matumizi.

 *Taarifa hii imetolewa na:* 

David Mramba,

Katibu wa Siasa na Uenezi CCM,

Mkoa wa Pwani.

No comments