Kamati ya siasa mkoa wa Pwani imeendelea kukagua miradi ya maendeleo wilaya Kibaha
Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Pwani chini ya Mwenyekiti wake *ndugu* *Mwinshehe* *Mlao* leo *tarehe 17/11/2023* imeendelea na ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo iliyopo ndani ya Mkoa wa Pwani.
Katika Wilaya hiyo ya Kibaha yenye majimbo mawili Kibaha Mjini na Kibaha Vijijini ambapo kwa ujumla wake Kamati hiyo ya Siasa Mkoa imeweza kukagua miradi ipatayo sita huku Jimbo la Kibaha Vijijini limekaguliwa miradi ya Bandari ya nchi kavu, Sino Tan Industrial Park iliyopo Kwala na Hospitali ya Wilaya iliyopo Disunyala.
Meneja msaidizi wa mradi wa Bandari Kavu Kwala *ndg. Gabriel* *Mwangosi* amesema lengo la kuanzishwa kwa bandari hiyo ni kupunguza asilimia 30 ya msongamano wa makontena katika
Bandari ya Dar -es
-Salaam na kutengeneza Mazingira mazuri ya huduma za Bandari kwa wateja wao hususani mataifa mbalimbali yanayohudumiwa na Bandari ya Dar -es - Salaam.
"Kinachotakiwa Bandari iwe inapumua kwa makontena mengine kuondolewa na kuruhusu makontena mengine Kuingia, ambapo itasaidia uharaka wa kupakua makontena kwenye meli na unapotaka kupima ubora wa Bandari ni kushusha haraka na kupakia haraka ili dhamira ya Serikali na Chama itimie" alisema *Mwangosi.*
*Ndg. Mwangosi* amesema katika eneo hilo la Kwala wanategemea kuwa na viwanda 250 ambapo mizigo itachukuliwa na kutokea Kwala na kupelekwa kwa wahusika ndani na nje ya nchi.
Ameendelea kusema kuwa yale mataifa yanayohudumiwa na Bandari ya DSM kama nchi yamepewa maeneo yao katika eneo hilo la Bandari Kavu ya Kwala ambazo ni nchi za Rwanda, Zambia, Congo lengo likiwa ni kushusha makontena 3000 kwa Siku sawa na Makontena laki 8 kwa mwezi.
Akizungumzia kuhusu mradi wa Kongani ya Viwanda Mwenyekiti wa SINO TAN *ndg Jauson* *Huang* amesema mradi huo ulianza mwezi may 2022 huku ukiwa na awamu tatu hadi kukamilika, ingawa awamu ya kwanza inatarajia kumalizika mwezi Desemba 2023.
*Ndg. Huang* ameendelea kusema kuwa mradi huo utakapokamilika utatoa faida ya kuajiriwa kwa wafanyakazi laki 1.
Aidha Kamati hiyo ilitembelea na kukagua huduma zinazotolewa katika Hospitali ya Wilaya ya Kibaha.
Hata hivyo Hospitali hiyo ili iweze kutoa huduma kwa ufanisi inahitaji kuwa na korido zinazounganisha jengo Moja kwenda jingine yenye urefu wa MITA 915 kufanya zaidi ya milioni 523 zinahitajika ili kukamilisha mpango huo.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Kibaha *Dr. Christopher* *Ngendello* amesema hadi kufikia October, 2023 jumla ya wagonjwa 5272 wamehudumiwa katika Hospitali hiyo.
Akizungumzia tangu kuanza kwa huduma ya X Ray na Ultra Sound Hospitalini hapo kumepunguza Idadi ya Rufaa zinazoenda Hospitali ya Mkoa ya Tumbi na kuweza kutibiwa Hospitalini hapo ambapo wagonjwa waliopatiwa huduma ni 759, kati Yao X ray ni 589 na Ultra sound 170.
Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Pwani ikiwa katika Halmashauri ya Mji Kibaha ilifanikiwa kutembelea na kukagua Utekelezaji wa Ilani Katika miradi ya Shule mpya ya Sekondari ya Shimbo Mkuza, Ujenzi wa barabara kwa kiwango Cha lami yenye urefu wa Km. 0.7 iliyopo picha ya ndege - Bokotimiza yenye thamani ya Shilingi bilioni 1 kupitia tozo za mafuta, na Soko la Kisasa lililopo katika Kata ya Tangini ambalo limekamilika kwa asilimia 99.5 na kugharimu jumla ya shilingi bilioni 8.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani *NDG* *Mwinshehe Mlao* amewataka Wazazi wa wazawa wa Mkoa wa Pwani kujikita zaidi katika kusomesha watoto wao ili waweze kunufaika na fursa za uwekezaji unaoendelea Mkoani Pwani.
*Ndg. Mlao* amesema Serikali tayari imetimiza wajibu wake wa kujenga Miundo Mbinu ya elimu kilichobaki ni Wazazi kuwapatia elimu watoto wao.
Ameendelea kusema kuwa kazi kuu ya mtoto ni kumsomesha na si kumfisadi kwa kumpatia kazi ambazo zitamwingiza kwenye vitendo vitakavyomkatiza masomo yake.
Alimalizia kwa kumpongeza Mhe. Daktari Samia Suluhu Hassan Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuonyesha Uzalendo wa kulithamini Taifa lake kwa kutoa fedha nyingi zinazotekeleza miradi ya maendeleo.

Post a Comment