Jshi la Israel lavamia hospitali ya Al-Shifa, lawakosa mateka - Netanyahu
Waziiri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amesema vikosi vya jeshi lake vilivania hospital ya Al Shifa huko Gaza, lakini likawakosa mateka wanaoshikiliwa na kikundi cha Hamas.
Israel imekuwa ikikishutumu kikundi hicho kuendesha harakati za kijeshi katika eneo la Hospitali hiyo, lakini Hamas wamekuwa wakikanusha mara kwa mara.
Mamia ya miili ya wapalestina walikuwa wamelundikana hospitalini hapo kufuatia mfululizo wa mashambulizi ya mabomu kutoka Israel ambao wamejibu mapigo ya uvamizi wa Hamas hapo Oktoba 7 mwaka huu.

Post a Comment