Israel yamrudisha nyumbani balozi wake kutoka Afrika Kusini
Israel imemrudisha nyumbani balozi wake wa Afrika Kusini "kwa mashauriano," Waziri wa mambo ya nje wa Israel, Lior Haiat amesema kupitia X bila kutoa maelezo zaidi.
Afrika Kusini imekuwa ikikosoa vikali operesheni ya kijeshi ya Israel huko Gaza. Siku ya Jumatatu iliitaka Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kutoa hati ya kukamatwa kwa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kabla ya kufika katikati ya Disemba.
Kuondolewa kwa Balozi wa Israel, Eliav Belotserkovsky kunakuja muda mfupi kabla ya Afrika Kusini kuwa mwenyeji wa mkutano kuhusu vita vya Israel na Hamas wa kundi la mataifa ya Brics, linalojumuisha China na Urusi.
Pia siku ya Jumanne, bunge la Afrika Kusini linatarajiwa kupiga kura kuhusu kufunga ubalozi wa Israel na kusimamisha uhusiano wote wa kidiplomasia hadi Israel itakapokubali kusitisha mapigano na kukubali kufanya mazungumzo yatakayo simamiwa na Umoja wa Mataifa.

Post a Comment