Hamas": Wapalestina 150 wataachiliwa kutoka jela za Israel chini ya makubaliano

 


Tumekuwa tukisikia kutoka kwa Israeli kuhusu mkataba wa mateka uliotiwa saini na baraza la mawaziri muda mfupi uliopita. Hamas pia imetoa taarifa kuhusu makubaliano hayo.

Taarifa hiyo iliyochapishwa kupitia Kituo cha Habari cha Palestina ambacho kimebeba taarifa rasmi za kundi hilo, ilisema mateka hao 50 wataachiliwa kwa kubadilishana na wanawake na watoto 150 wa Kipalestina wanaozuiliwa katika jela za Israel.

Mkataba huo pia utaruhusu mamia ya malori yanayobeba misaada ya kibinadamu, vifaa vya matibabu na mafuta kuingia Gaza, kulingana na Hamas.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa Israel ilisema haitashambulia wala kumkamata mtu yeyote huko Gaza wakati wa kusitisha mapigano.

Na ilisema kuwa ndege wakati wa mapumziko ya siku nne, hazitapaa kabisa kusini mwa Gaza kwa saa sita kwa siku, kutoka 10:00 hadi 16:00 kwa saa za ndani, kaskazini mwa Gaza.

Hamas, ambayo inachukuliwa kuwa kundi la kigaidi na nchi nyingi ikiwa ni pamoja na Uingereza na Marekani, iliteka nyara karibu watu 240 kutoka Israeli wakati wa mashambulizi yake ya kikatili tarehe 7 Oktoba.


No comments