Binti wa mateka wa Hamas anaelezea 'kiza kinene'
Binti ya watu wawili waliochukuliwa mateka na Hamas tarehe 7 Oktoba amezungumza na BBC Newsnight baada ya kurejea Uingereza kutoka Israel.
Mamake Sharone Lifschitz, Yocheved, 85, aliachiliwa wiki mbili zilizopita - babake, Oded, 83, bado hajulikani alipo.
Sharone alielezea mama yake kama "mwale wa mwanga", lakini alisema pia kuna "kiza kinene", na kwamba bado anasubiri habari kuhusu baba yake.
“Hata sijui amefariki au yuko hai. Tunajua alijeruhiwa, tunajua amepigwa risasi, lakini hatujui kama alinusurika,” alisema.
Alitoa wito kwa mateka wanaoshikiliwa na Hamas kuachiliwa, na pia alielezea "mateso ya watoto" wa Ukanda wa Gaza kama "ya kutisha".
"Binadamu yeyote ataona jambo hilo kuwa la kutisha kwa sababu tunashirikishana ubinadamu," alisema, akiongeza kwamba alitaka jamii "zielekee katika uwezekano wa kuishi pamoja".

Post a Comment