Waziri Mkuu wa Uingereza alaani 'ugaidi wa kuogofya' alipowasili Israel

 

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak amewasili Israel na kuwaambia waandishi wa habari katika uwanja wa ndege wa Tel Aviv kwamba mashambulizi ya Hamas tarehe 7 Oktoba yalikuwa "tendo la kigaidi lisiloelezeka", na akasisitiza kwamba Uingereza inasimama pamoja na Israel.

"Nasubiri sana mikutano yangu baadaye na waziri mkuu na rais na ninatumai sana itakuwa mikutano yenye tija," Sunak amesema.


No comments