SIMBA KUIVAA AL AHYL KESHO, MSANII MKUBWA KUTUMBUIZA UFUNGUZI
MECHI ya ufunguzi wa michuano mikubwa zaidi barani Afrika, African Football League itapigwa kesho katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, saa 12.30 jioni kati ya wenyeji Simba dhidi ya mabingwa wa kihistoria barani Afrika, Al Ahyl ya Misri.
Ni mechi inayotazamiwa kutazamwa zaidi Afrika kwa ngazi ya Klabu katika historia, kwani licha ya uwepo wa Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Patrice Motsepe, atakuwepo pia bosi wa FIFA, Giani Ifantino, kocha mwenye heshima kubwa duniani, Arsene Wenger pamoja na marai wa vyama mbalimbali vya soka duniani.
Ni mechi yenye hadhi ya kipekee, serikali ikitumia zaidi ya shilingi bilioni 30 kwa ajili ya ukarabati mkubwa, vikiwekwa viti vipya, taa mpya na za kisasa na matengenezo ya vyumba vya kubadilishia nguo, eneo la kuchezea (pitch).
Ndani ya Uwanja, Simba ambayo inaongoza Ligi Kuu Tanzania Bara, inatarajiwa kuwa na wakati mgumu dhidi ya mabingwa hao wa Afrika, kwani baada ya mechi hiyo, watalazimika kusafiri hadi Cairo, kucheza mechi ya pili itakayoruhusu mshindi wa jumla kuingia nusu fainali, katika michuano hiyo inayoshirikisha miamba wanane bora zaidi kisoka barani.


Post a Comment