MTOTO WA BILIONEA AKIRI KUHUSIKA MAUAJI YA MWANAFUNZI WA KIKE
Farouk Abd al-Haq, ambaye ni mtoto wa kiume wa bilionea wa Kiarabu, akizungumza na Shirila la Utangazaji la Uingereza (BBC), amekiri kuhusika katika mauaji ya msichana Martine Vic Magnussen aliyekuwa na umri wa miaka 23 mwaka 2008.
Farouk ambaye alikimbilia Yemen saa
chache baada ya mauaji ya mwanafunzi huko London miaka kumi na tano iliyopita,
amekiri kwa BBC kwamba alihusika katika mauaji yake.
Mwili wa Martin Vic Magnussen, uligunduliwa ukiwa umefukiwa chini ya vifusi katika sehemu ya chini ya nyumba
kwenye Mtaa wa Great Portland mwaka wa 2008.
Tangu wakati huo, familia yake imekuwa ikitafuta haki. Farouk Abd al-Haq, ambaye anaongoza katika orodha inayosakwa na polisi wa Uingereza, na ambaye hati ya kimataifa ya kukamatwa kwake imetolewa, hajawahi kuzungumza katika kesi hii.
Aliambia BBC kwamba kifo cha Martin Vik Magnussen kilitokana na 'ajali ya ngono iliyokwenda mrama'.
Hata hivyo, Abdul Haq, ambaye alisoma na Vic Magnussen, pia
alisema hayuko tayari kurejea Uingereza kuzungumza na polisi, kwa kuwa 'amechelewa'.
"Nilikuwa mwanafunzi wakati mwili wa Martine ulipopatikana, na
nilipata mshtuko mkubwa, haswa wakati niliposikia madai kuwa mshukiwa mkubwa wa
mauaji yake alikuwa Myemen - na mimi pia natoka Yemen.
Kwa hiyo simulizi hii ilikuwa moja ya nilizozipa kipaumbele
nilipojiunga na BBC kama mwandishi wa habari mwaka wa 2011.
Lengo langu kuu wakati huo lilikuwa kupata majibu kutoka kwa
familia ya Martine, wanaoona mauaji yake kama mtihani wa sheria za kimataifa,
hasa kwa vile hakuna makubaliano kati ya Uingereza na Yemen ya kubadilishana
wafungwa na wale waliofunguliwa mashtaka kisheria.
Hata hivyo, sikuweza kuwasiliana na Farouk Abdelhak hadi mwaka
jana.
Nilianza kuwasiliana naye kwenye mitandao ya kijamii.
Mamia ya waandishi wa habari wamejaribu kuwasiliana naye katika
kipindi cha miaka kumi na minne iliyopita, lakini amewapuuza wote.
Hata hivyo, malezi yetu ya pamoja ya Wayemeni yalinisaidia
kupata imani yake.
Baada ya siku kumi za mawasiliano kati yetu, alinitumia ujumbe
wa kwanza ambao ungebadilika na kuwa jumbe nyingi za ufichuzi.
"Nilifanya jambo nilipokuwa mdogo, na lilikuwa kosa,"
aliandika katika mojawapo ya barua hizo.
Kupitia maelfu ya ujumbe wa maandishi na maelezo ya sauti
aliyonitumia kwa muda wa miezi mitano, hakuwahi kutumia jina la Martine, wala
hakurejelea kifo chake, akipendelea kutumia neno 'ajali.'
Hata hivyo, ripoti ya kitaalamu ilifafanua maelezo ya kifo cha
kikatili cha mwanafunzi huyo wa Norway - kutokana na kushinikizo shingoni,
ambayo ina maana kwamba 'huenda alinyongwa, kubanwa chini kwa nguvu na
kushindwa kupumua.'
Mwili wake ulikuwa na majeraha na mikwaruzo 43 aliyopata, 'baadhi ya hayo yanaonyesha wazi kuwa alishambuliwa au aliyopata wakati wanakabiliana.'
Farouk na Martine wote walisoma katika Shule ya Biashara ya
Regent huko London, na Martine alitarajia kupata kazi katika sekta ya fedha na
biashara katika mji mkuu.
Mara ya mwisho marafiki zake walimwona akiwa hai ilikuwa mapema
Machi 14, 2008, katika klabu ya usiku ya kipekee ya Maddox huko Mayfair London,
ambapo yeye na Farouk walikuwa wakisherehekea kumalizika kwa mitihani.
Marafiki wanasema kuwa Farouk alijitolea kuandaa tafrija katika
nyumba yake kwenye Mtaa wa Great Portland katikati mwa London.
Marafiki walikuwa wamechoka, lakini wanasema Martine alitaka
kuendelea kusherehekea - kamera za usalama zinaonyesha aliondoka na Farouk saa
2:59 asubuhi. Hakuna mashahidi wa kilichotokea baadaye.
Na kabla ya jua kuchomoza, Martine alikuwa ameaga dunia - ingawa
mwili wake haukugunduliwa hadi baada ya saa 48 baadaye.
Kufikia wakati huo, Farouk alikuwa ameondoka Uingereza kwa ndege
kuelekea Cairo. Kisha akapanda ndege binafsi ya baba yake, kuelekea Yemen.
Wakili wake anasisitiza kuwa hana hatia ya mauaji hayo.
Farouk hakuwa raia wa kawaida wa Yemen. Alikulia kati ya
Marekani na Misri.
Yeye ni mtoto wa Shaher Abdulhak, - mmoja wa Wayemen tajiri
zaidi na wenye mamlaka nchini humo.
Alikuwa na himaya ya biashara ya sukari, vinywaji baridi, mafuta
na biashara ya silaha, na pia alikuwa rafiki wa karibu wa rais wa Yemeni wakati
huo, Ali Abdullah Saleh.
Nilipojaribu kuwasiliana na Farouk kwa mara ya kwanza katika
mwaka wa 2011, nilitumia miezi mingi nchini Yemen kumtafuta. Lakini
nililazimika kuondoka mamlaka iliponiambia niachane na simulizi hiyo.
Mnamo Februari mwaka wa 2022, niliamua kusikiliza kesi hiyo tena, kutoka London. Wakati huo, Baba yake Farouk alikuwa amefariki na Rais Saleh alikuwa amepinduliwa. Nilijiuliza iwapo nitafanikiwa kumtafuta Farouk aongee.
Lakini pia nilijua haingekuwa rahisi. Rafiki yangu alipofanikiwa
kupata nambari yake, nilimtumia ujumbe mfupi wa maandishi kwa kutumia programu
nyingi za simu, lakini hakujibu. Kisha rafiki yangu akagundua kuwa Farouk
alikuwa akitumia Snapchat.



Post a Comment