MRUSI ATIMULIWA INDONESIA KWA KUKAA UCHI MLIMA MTAKATIFU
Mwanaume
mmoja raia wa Russia ametimuliwa nchini Indonesia baada ya kubainika kuvua nguo
zake na kubaki uchi wa mnyama katika Mlima Agung ambao unaabudiwa kama Mlima
Mtakatifu.
Mwanamume
huyo aliyetambulika kwa jina moja la Yuri, ameomba msamaha lakini atazuiwa
kuingia tena Indonesia kwa angalau miezi sita.
Indonesia
ambayo Mji wake mkuu ni Bali, hivi karibuni imeongeza juhudi za kukabiliana na
watalii wa kigeni wanaotajwa kukosa maadili.
Mlima
Agung, sehemu ya juu zaidi katika kisiwa hicho, inaaminika na Wahindu kuwa
makao ya miungu. Afisa wa eneo alisema ‘hakuna kisingizio’ kwa tabia yake.
"Alikiuka
kanuni na hakuonyesha heshima kwa utamaduni wetu," Mkuu wa Ofisi ya Sheria
na Haki za Kibinadamu ya Bali, Anggiat Napitupulu aliambia Jakarta Post.
Katika
video iliyowekwa kwenye Instagram kwa lugha ya Kirusi, Yuri alisema:
"Kitendo changu hakina kisingizio. Kitu pekee kilichosababisha
kilichotokea ni ujinga wangu binafsi."
Baadaye
alishiriki katika hafla maalum ya utakaso wa mlima huo - tambiko ambalo mara
nyingi hufanyika na wenyeji baada ya matukio kama haya.
Wijaya,
balozi mdogo wa heshima wa Urusi huko Bali, aliiambia CNN Indonesia kwamba
mtalii huyo alikuwa ‘mwehu’ na kwamba kumfukuza ni jambo sahihi kufanya.
Wenyeji wengi kwenye mitandao ya kijamii pia waliunga mkono kufukuzwa kwake.


Post a Comment