RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI WIZARA YA MAMBO YA NJE
Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa mabalozi kadhaa kuunda Kamati Maalum ya Kutathmini Utendaji kazi wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ili kuiwezesha wizara hiyo kutekeleza malengo ya serikali katika kukuza diplomasia ya uchumi na ushirikiano wa kimataifa.
Balozi Yahya Simba, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Zambia, ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo na kuwateua wengine kuwa wajumbe wa Kamati.
Wajumbe hao wa Kamati ni Ramadhani Mwombe Mwinyi, ambaye ni Kastibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu wa Zanzibar, Balozi Mwanaidi Sinare Majaar, aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Balozi Allan Peter Kalaghe aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini Uingereza na Tovako Nathaniel Manongi, aliyekuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, New York nchini Marekani.


Post a Comment