ASKOFU MALASUSA ATAKA SHULE ZA KANISA ZIITWE ZA KIROHO, SIYO ZA BINAFSI
Askofu kiongozi wa Kanisa la KKKT, Alex Malasusa ameitaka jamii kuacha kuziita shule zinazomilikiwa na taasisi za kidini kuwa ni za binafsi na badala yake ametaka ziitwe za kiroho.
Askofu Malasusa alitoa rai hiyo leo wakati akishiriki katika sherehe za miaka 30 ya Shule ya Sekondari ya Kisarawe ya Mkoani Pwani, iliyofanyika Mkuza Kibaha.
"Shule za kanisa hazifanyi biashara, ada yake ni ndogo tofauti na shule za binafsi ambazo nyingine hutoza ada hadi shilingi milioni 9 kwa mwaka," alisema.
Hata hivyo, katika baadhi ya mitandao ya kijamii, baadhi ya wachangiaji walipingana naye, wakisema shule nyingi za makanisa zimekuwa zikitoza ada kubwa kuliko hata za binafsi.

Post a Comment