DROO YA UEFA YATOLEWA, VIGOGO NANE DIMBANI, REAL SAFARINI KUTWAA UBINGWA WA 15
Shirikisho la Soka Barani Ulaya limechezesha droo ya miamba nane iliyosalia katika michuano ya Ligi ya Mabingwa msimu huu, likitoa nafasi kwa mabingwa wa kihistoria Real Madrid kutwaa taji lao la 15.
Madrid wataumana na Chelsea katika robo fainali na endapo wataipiga timu hiyo inayochechemea katika Ligi Kuu England msimu huu, watakutana na mshindi kati ya wataliano wawili, Napoli itakayocheza dhidi ya AC Milan.
Mechi zingine za robo fainali ni kati ya miamba wa Ujerumani, Bayern Munich dhidi ya Man City wanaofundishwa na kocha wa zamani wa mabingwa hao wa Bundesliga, Pep Gardiola.
Na vinara wa Ligi Kuu nchini Ureno, Benfica watajaribu kuingia nusu fainali wakitafuta namna ya kuichapa Inter Milan ya Italia.

Post a Comment