LESOTHO YATAKA MIJI YA AFRIKA KUSINI KUREJEA KATIKA MIPAKA YAKE



Bunge la Lesotho linatarajiwa siku ya Jumatano kujadili hoja kuhusu kurejeshwa kwa baadhi ya maeneo ya Afrika Kusini chini ya himaya yake.

Mbunge wa upinzani anataka wabunge "kutangaza eneo lote la Free State, sehemu za Rasi ya Kaskazini, sehemu za Rasi ya Mashariki, sehemu za Mpumalanga na sehemu za KwaZulu-Natal kama sehemu ya eneo la Lesotho", kulingana na karatasi ya agizo la bunge.

Inasema urejeshaji huo utatekelezwa chini ya Azimio nambari 1817 la Umoja wa Mataifa (XVII) ambalo lilipitishwa na Baraza Kuu mnamo Desemba 1962.

Kihistoria, watu wa Lesotho walipatikana katika Orange Free State ya Afrika Kusini, Eastern Cape, Northern Cape, Mpumalanga na sehemu za KwaZulu-Natal.

Lakini walilazimishwa kuhamia Lesotho ya sasa kwa sababu ya vita.

  

No comments