KAMATI YA MIUNDOMBINU YAHIMIZA NGUVU ZAIDI TAASISIYA TEKNOLOJIA YA UJENZI - ICoT

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu  imeiagiza Wizara yaUjenzi na Uchukuzi, kuongeza nguvu kwenye Taasisi ya Teknolojia yaUjenzi (ICoT), kwa kuitengea fedha za kutosha ili iweze kujiendelezakwa kuwa na vifaa na mitambo ya kisasa, vitendea kazi, majengo narasilimali   watu   kwa   ajili   ya   kuwezesha     kuzalisha   mafundi   wenyeuwezo na ujuzi.

Hayo yamesemwa mkoani Morogoro na Mwenyekiti wa Kamati hiyo,Mhe. Selemani Kakoso, mara baada ya kupokea taarifa ya Taasisi hiyo iliyoanzishwa   kwa   kuunganisha   Chuo   cha   Taifa   cha   Ujenzi   cha Morogoro na Chuo cha Teknolojia stahiki ya nguvu kazi cha Mbeya na kusisitiza uhitaji wa  taasisi hiyo kuongezewa bajeti.

“Kamati   inaomba   Wizara   muwe   na   dhamira  ya   dhati   ya   kukisaidia Chuo   hiki   ili   kiweze   kuimarika   kwani   kufanya   hivyo   mtazalisha waatalamu wa kutosha wenye ujuzi na uwezo wa  kufanya kazi kwavitendo kwa kutumia teknolojia stahiki,”amesema Mhe. Kakoso. 

Aidha, Kamati hiyo imesisitiza kuwa Taifa linategemea sana vyuo hivyo kwani ndio msingi wa kupata mafundi wa ngazi ya kati na kuendeleza kusimamia na kuboresha miradi ya barabara na reli inayoendelea.Kamati imeiagiza Wizara kuhakikisha Taasisi hiyo inapata wakufunzi wa kutosha wa fani zote ili kuongeza nguvu na ujuzi kwa wanafunzi watakaopata   fursa   ya   kujiendeleza   katika   Taasisi  hiyo   na   kusaidia Chuo kuongeza kutambulika zaidi.

Awali akitoa taarifa kwa Kamati, Mkuu wa Taasisi hiyo Eng. MahmoudChamle, ameieleza kamati kuwa uanzishwaji wa taasisi hii utachangiakupunguza   changamoto   ya   ukosefu   wa   ajira   kwa   vijana   kwani mafunzo yanayotolewa hapo yatawaandaa wahitimu kujiajiri zaidi.

Ameongeza kuwa Taasisi yake inatoa mafunzo ya muda mrefu katika fani  za  ujenzi,   umeme,   na  mitambo  katika   ngazi  ya  Astashahda  na Stashahada   lakini   pia   inatoa   mafunzo   ya   muda   mfupi   na   mafunzo maalum   kwa   wahitimu   wa   fani   za   kihandisi   na   zinazoendana   ilikuwaandaa na kuwajengea uwezo.

Ameendelea kusema kuwa kwa sasa Taasisi inaendesha mafunzo juu ya matumizi ya Teknolojia Stahiki ya Nguvu kazi katika kazi za ujenzi, matengenezo na ukarabati wa barabara.

Kamati ya Miundombinu ipo mkoani Morogoro katika ziara yake ya kukagua miradi na kazi zinazofanywa na taasisi zilizo chini ya Wizaraya Ujenzi na Uchukuzi.


No comments