PAPE OSMANE SAKO AITWA TIMU YA TAIFA YA SENEGAL

Kocha wa Timu ya Taifa ya Senegal, Khalou Cisse ambaye alikiongoza kikosi hicho katika fainali za kombe la dunia huko Qatar, amemuita kiungo mshambuliaji wa Simba, Pape Osmane Sakho.

Sakho, aliyejiunga na Simba msimu uliopita, anaitwa kwa mara ya kwanza kujiunga na kikosi hicho kitakachojiwinda kwa ajili ya kusaka kucheza fainali za Afcon 2023, katika mchezo dhidi ya Msumbiji.

Anakwenda kujiunga na nahodha wake Saido Mane anayeichezea Buyern Munich ya Ujerumani ambako wachezaji asilimia tisini wanasakata kabumbu barani Ulaya.

No comments