WAZAZI WAWAFELISHA WATOTO ILI WAKAWA MAHAUSIGELI

Wazazi na walezi Wilayani Lushoto mkoani Tanga wanawashawishi watoto wao walio mashuleni kufeli makusudi kusudi wasiendelee na masomo na badala yake waende kufanya kazi za ndani.

Ukweli huo umefichuliwa na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Tanga, Husna Sekiboko aliyekuwa katika ziara ya Tarafa kwa Tarafa ili kuona utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi.

Aliaema amepata taarifa kwamba wapo baadhi ya wazazi na walezi wamekuwa wakiwashawishi watoto wao kufanya vibaya katika mitihani yao ili wasiendelee na masomo na badala yake wakafanya kazi za ndani kwa matajiri ndani na nje ya wilaya hiyo.

Akiwa ni Makamu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi Husna alisema wazazi wanatakiwa kuwahamasisha watoto kufanya vizuri katika masomo yao kwani elimu ni muhimu katika maisha yao ya sasa na baadaye.

No comments