TIMU YA SIMON MSUVA HATARINI KUSHUKA DARAJA
Timu ya soka ya Al-Quadsiah,inayoshiriki Ligi Kuu nchini Morocco, ambayo Mtanzania Simon Msuva anaichezea, ipo hatarini kushuka daraja.
Ikiwa na alama 22 kibindoni, timu hiyo imebakiwa na mechi tatu mkononi na ili ibakie inapaswa kushinda mechi hizo zote kwani timu tatu zilizo chini yake, zina pointi chini ya 20.
Msuva ambaye amefunga mabao saba katika mechi saba alizoichezea timu hiyo, alisema anajihisi mwenye deni kubwa kwani asingependa kuwa na historia ya kushuka na timu daraja.

Post a Comment