TAMASHA LA PASAKA LAREJEA TENA

Tamasha la Pasaka, moja kati ya matukio makubwa ya kiburudani nchini, ambalo lilisimama kwa muda wa miaka saba,limerejea tena ulingoni.

Mkurugenzi wa Msama Promotions ambao ndiyo waandaaji, Alex Msama alisema jijini Dar es Salaam kwamba baada ya kuwa kimya kwa muda huo, sasa limerejea na litafanyika mwaka huu.

Tamasha hilo kubwa kabisa la nyimbo za Injili nchini, hushirikisha waimbaji kutoka ndani na nje ya nchi ambao ni maarufu.

No comments