SIMON MSUVA AWAAMBIA SIMBA: HAO RAJA MSIWACHUKULIE POA, WANAJUA

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva, amewatahadharisha Simba kutoichukulia poa timu ya Raja Cansablanca ambayo inakutana nayo kesho Jumamosi katika mchezo wa pili wa hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Msuva, mchezaji wa zamani wa Yanga ambaye alipata kuichezea Wydad, wapinzani wakubwa wa Raja,  alisema timu hiyo ni nzuri katika kucheza mchezo wa kupoteza muda na endapo Mnyama atatanguliwa kufungwa, basi itakuwa mechi ngumu kwao.

Aliwataka Simba kuwa makini katika mchezo huo, kwani alimkumbuka mchezaji mmoja matata aitwaye Yusuf  ambaye bado yupo na timu hiyo kuwa ni mchezaji wa kuchungwa.

Simba na Raja Cansablanca zinakutana kesho saa moja usiku katika dimba la Benjamin Mkapa, huku wageni wakiongoza kundi lao baada ya kushinda mechi yao ya kwanza kwa kuipiga Vipers ya Uganda mabao5-0,  wakati Simba alichezea kichapo cha bao 1-0 akiwa ugenini dhidi ya Horoya jijini Conakry.

No comments