RASMI: FEI TOTO KUIVAA TP MAZEMBE KESHOKUTWA
Baada ya kukurukakara za muda mrefu, minong'ono na tetesi na taarifa zisizo rasmi, hatimaye uongozi wa Yanga leo umewaambia Wananchi kuwa Jumapili hii, The Zanzibar Finest, atakuwa dimbani kuwakabili Mabingwa mara tano wa Afrika, TP Mazembe.
Ali Kamwe, Msemaji wa mabingwa wa kihistoria nchini, Yanga, aliwaambia waandishi wa habari leo kuwa Feisal Salum atakuwa sehemu ya kikosi kama kocha ataona inafaa, maana kila kitu kipo vizuri.
Amesema uongozi umemalizana na Fei Toto ambaye amekubali kurejea kundini baada ya kususa kuichezea timu hiyo akilalamikia masilahi madogo, akipinga kulipwa shilingi milioni 4 kwa mwezi, tofauti na wanavyolipwa wachezaji wengine, akiamini mchango wake ni mkubwa kuliko wao.
Japo Kamwe hakuingia kwa undani juu ya uboreshwaji wa mkataba wa kiungo huyo mshambuliaji, inadaiwa kuwa uongozi wa Yanga umeboresha mkataba wa miaka miwili kwa kumpa mshahara wa shilingi milioni 15 kwa mwezi.

Post a Comment