SERIKALI YASISITIZA USHIRIKIANO NA AFDB

.​

Serikali imesema itaendeleza ushirikiano kati yake na wadau wa maendeleo katika kuboresha miundombinu mbalimbali ya maendeleo.

Kauli hiyo imetolewa leo na  Waziri wa  Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa wakati akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Kanda ya Afrika Mashariki na Kati wa Benki ya Afrika (AFDB), Jonatahari  Nzayikorera, akisema lengo la serikali ni kuona miundombinu bora inayoweza kutumika kwa vipindi vyote vya mwaka.

Alisema serikali inafurahi kuona wafadhili wakifika kuona fedha wanazotoa zinavyotumika kwa macho yao wenyewe. Alitoa maneno hayo wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato jijini Dodoma.

Profesa Mbarawa ametumia fursa hiyo kumtaka mkandarasi kuongeza vifaa vya kazi ili kazi hiyo imalizike kwa wakati na viwango vilivyokubalika.


No comments