CHAMA, AZIZ KI WALAMBA MKATABA CRDB, PIA WAZAWA ZIMBWE JUNIOR, FARID MUSSA WAMO

Wachezaji wawili wageni wa kimataifa wa klabu za Simba na Yanga, Clatous Chota Chama na Stephano Aziz Ki, wamelamba dume baada ya kuingia mkataba na Benki ya CRDB.

Katika mkataba uliosainiwa leo, pia wachezaji wazawa, Farid Mussa Malik wa Yanga na Mohammed Hussein 'Zimbwe Jr' wa Simba, nao walijikuta wakipata donge nono.

Wachezaji hao walisaini mkataba wa kuwa mabalozi wa kutoa elimu ya matumizi ya Simbank

ing ya benk hiyo inayofanya vizuri nchini Tanzania kwa sasa.



Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Nsekela alisema lengo ni kuwatumia wanasoka hao kusambaza elimu juu ya matumizi mazuri ya Simbanking.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu wa timu hizo, sambamba  a mabosi wa CRDB.


No comments