RAIS AFRIKA KUSINI AKATAA RAPA AKA KUZIKWA KITAIFA
Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amekataa ombi la serikali ya mji na familia kutaka rapa, AKA azikwe kwa heshima za kitaifa.
Panyaza Lesufi, kiongozi wa Gauteng, mji wenye matukio mengi ya kihalifu, alipeleka ombi kwa Rais Ramaphosa kutaka kijana huyo azikwe kwa heshima ya jeneza lake kufunikwa bendera ya Taifa hiku wakitaka pia ipepee nusu mlingoti.
Rais amekataa ombi hilo na sasa mwanamuziki huyo atazikwa kwa faragha na familia yake hapo kesho na leo itafanyika misa maalum kwa ajili yake.
Kienan Forbes, aliuawa kwa kupigwa risasi usiku wa Ijumaa, Februari 10 mwaka huu, katika Mgahawa wa Wish, Barabara ya Florida, huko Durban Kwa Zulu Natal akiwa na rafiki yake, mjasiriamali na mpishi maarufu, Tebele Motsoane.

Post a Comment