PANYA ROAD WAMNING'INIZA MTOTO MBELE YA WAZAZI WATISHIA KUMKATA MAPANGA WASIOOTOA FEDHA
Wahalifu vijana maarufu kama Panya Road ambao walitoweka kufuatia operesheni kali ya polisi wakati wa Rais John Magufuli, wamerejea tena kwa kishindo na safari hii, katika eneo la Bunju jijini Dar es Salaam waliwajeruhi kwa kuwakata mapanga watu kadhaa.
Leo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema wahalifu watano wamekamatwa, sambamba na vitu mbalimbali walivyoiba.
Mmoja wa wahanga wa tukio hilo aliyyejitambulisha kwa jina moja la Britness, alisema wahalifu hao baada ya kuvunja mlango na kuingia ndani kwao, walimchukua mtoto mdogo na kumning'iniza juu, wakiwataka wazazi kutoa fedha, simu na kompyuta mpakato, vinginevyo watamkata mapanga.
Baada ya kupewa vitu hivyo, walimtaka pia dada wa familia hiyo kuvua nguo ili wambake, lakini akakataa.
Katika kile kinachoonekana kama hofu ya Polisi kushambuliwa na panya road hao, Kamanda Murilo ametoa onyo kuwa shambulio lolote dhidi ya polisi litajibiwa vikali, huku akiweka wazi kuwa wasije kulaumiwa.

Post a Comment