RAIS SAMIA ATAKA WANACHUO KUPIGA KITABU, WAACHANE NA STRESS ZA MAPENZI
Rais Samia Suluhu Hassan ambaye jana aliongeza boom kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, amewataka vijana hao kujihusisha zaidi na kuachana na mambo ya mapenzi.
Alisema wapo wanafunzi ambao badala ya kuww bize na masomo, wamekuwa wakijihusisha na mapenzi kiasi cha kupeana stress, kitu ambacho alisema hakina tija, kwani maisha yao ni zawadi pekee kutoka kwa Mungu.
"Yaani unasoma halafu kuna lijitu huko eti linakusumbua, anasema nitakufa juu yako, ukimwambia akafe haendi, jali yaisha yako ya sasa, kwani hayo mambo mengine tutakutana nayo mbele ya safari."

Post a Comment