PROFESA IBRAHIM LIPUMBA APATA AJALI
Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amepata ajali jana, baada ya gari lake kupinduka na kuharibika vibaya katika eneo la Nangurukuru mkoani Lindi.
Profesa alikuwa katika shughuli za kisiasa, akiwa ametoka kuhutubia mkutano wa hadhara huko Kilwa Kivinje.
Mkurugenzi wa Habari na Mahusiano ya Umma wa chama hicho, Injinia Mohamed Ngulangwa amesema kiongozi huyo na watu wengine waliokuwemo ndani ya gari hilo wako salama, ila gari hilo limeharibika vibaya.

Post a Comment