MCHUNGAJI APOTEZA MAISHA AKIJARIBU KUIFIKIA REKODI YA YESU KRISTO

Mchungaji wa kanisa moja nchini Msumbiji, amepoteza maisha wakati akijaribu kuifikia rekodi ya Yesu Kristo,aliyefunga kwa siku 40 katika milima ya Mizeituni ya Biblia.

Fransisco Barajah, mchungaji mwanzilishi wa Kanisa la Kiinjili la Trindande alifariki baada ya kufikisha siku 25 za kufunga kwake ambapo hali yake ilianza kubadilika huku akipoteza uwezo wa kusimama,kuongea na mwili kupungua kwa kiasi kikubwa.

Waumini na ndugu zake walimchukua na kumpeleka hospitali, lakini madaktari walishindwa kuokoa maisha yake na ikaripotiwa jana kuwa ameaga dunia.

No comments