KUNA FLAMINGO MILIONI 2 ZIWA NATRON, NDEGE WENYE MAAJABU LUKUKI

Ndege aina ya Flamingo ana maajabu mengi yasiyofahamika, lakini jambo la kufurahisha ni kwamba wanyama hao ambao jina lao lina asili ya Hispania likimaanisha moto, wapo milioni mbili ndani ya Ziwa Natron ambalo lina maji chumvi.

Ziwa Natron lina ukubwa wa heka karibu 1400, ukubwa sawa na jiji lote la Dar es Salaam.

Flamingo ana maajabu kadhaa na miongoni mwa la kufurahisha ni kwamba hawajaamiiani hovyo. Hukaa na kusubiri hadi muda wa kupevuka unapofiika na ukifika, ndege hao wana tabia ya kucheza dansi ili kumvutia mwenza wake.

Na ikitokea amempata, basi huyo ndiye huwa mwenza wake wa milele. Hutaga yai moja tu kwa mwaka na katika kulipevusha, ndege hao mume na mke, wote hulilalia yai hilo kwa muda wa mwezi mmoja.

Vifaranga vya Flamingo hulishwa kwa chakula kinachotengenezwa kwenye makoo yao na umri wake wa kuishi, yaani lifespan, ni kati ya miaka 20 hadi 30.

Hata hivyo, historia inaonyesha kuwa Flamingo mmoja, aliishi kwa muda wa miaka 83, akiwa katika shamba la wanyama (zoo) ya Adelaide, iliyopo nchini Australia na alikufa mwaka 2014.

Sifa nyingine ya Flamingo ni uwezo wake wa kuhisi uwepo wa mvua umbali wa km 500, karibu sawa na umbali kutoka jijini Dar es Salaam hadi Iringa.

Ndege huyo pia anaweza kupaa umbali wa km 56 kwa saa na hutumia zaidi ya asilimia 30 ya muda wao kwa siku wakijisafisha mabawa yao.

Jambo la kustaabisha zaidi ni kuwa ndege hao wakitaka kupumzika, basi husimama kwa mguu mmoja na kwa kawaida, hupendelea na kuwa na amani wakitembea makundi makubwa.

No comments