NECTA YAONDOA TOP TEN, YASTUKIA PROMO

Baraza la mitihani Tanzania, limeondoa utaratibu wa kutangaza shule na

wanafunzi bora kwa kile ilichosema utaratibu huo hauna tija kwa nchi zaidi ya kuzitangaza shule.

Akizungumza Dar es Salaam leo wakati akitoa matokeo ya mitihani ya kidato cha nne kwa mwaka 2022, Kaimu Mtendaji Mkuu wa NECTA, Athumani Amasi, alisema siyo sawa kuwalinganisha wanafunzi wanaotoka katika mazingira tofauti, licha ya kufanya mitihani inayofanana.

Aidha Amasi amesema utaratibu wa kutangaza shule 10 Bora, ni kama kuzipromoti shule hizo, jambo ambalo Baraza limeona halina tija kwa sasa.

Kwa miaka mingi sasa, Baraza la Mitihani nchini, wakati wa kutangaza matokeo ya mitihani ya darasa la nne, la saba, kidato cha pili, kidato cha nne na sita, limekuwa pia likitangaza wanafunzi kumi bora kitaifa, sambamba na shule, ambapo mara nyingi zimekuwa zikinyakuliwa na shule binafsi.

No comments