JENGO LINALOPITISHA MABILIONI KILA MWAKA

Hili ni jengo la Chama Cha Ushirika Pilikano maarufu kama Pilikano Amcos, lina umri wa zaidi ya miaka mia.

Lipo katika Kijiji Cha Mkumbi, wilayani Mbinga Mkoa wa Ruvuma. Kijiji cha Mkumbi na karibu maeneo mengi ya wilayani Mbinga ni maarufu kwa kilimo cha Kahawa, moja ya kati ya mazao ya kimkakati nchini.

Wakulima wa zao hilo, hupitisha kahawa yao katika chama hiki na hesabu za mwaka jana, wakulima walilipwa zaidi ya milioni 1500 (1.5b).

Unapatwa na mshangao, kwa nini jengo lao licha ya kupitisha fedha nyingi kiasi hicho, bado halikarabatiwi liwe na sura ya kisasa.

Ojuku Blog iliongea na Mwenyekiti wa Amcos hiyo, Vicent Liborius Kapinga juu ya suala hilo na haya ndiyo yalikuwa majibu yake:

"Tumeshawaita wanachama na kuwaeleza juu ya kulikarabati jengo hili liwe la kisasa, lakini wanakataa. Tuliwapa bajeti, lakini wakakataa, tumeishia kulipaka rangi tu.."


No comments