FEDHA WANAZOPATA WATOTO WA BONGO FLEVA LEO, SUGU ALIZIONA MIAKA 30 ILIYOPITA

Naweza kuwa sina mawasiliano ya kivile na Joseph Mbilinyi, mkongwe wa muziki wa kizazi kipya, ambaye tunamfahamu kama Sugu, lakini hii hainizuii kuzungumza kuhusu mawazo yake 'those days'.

Sugu ni mdogo kwangu kiumri, lakini ana akili kubwa kuliko mimi. Siku ya kwanza kukutana nae, ilikuwa mwezi flan hivi, 2003, pale Kijitonyama jijini Dar es Salaam katika baa moja maarufu enzi hizo, iliyoathiriwa na upanuzi wa barabara ya Bagamoyo, ikiitwa Chaga Bite.

Nilikuwa na mdogo wangu, Alfred Lukas ambaye baadae alikuja kuwa ofiss habari wa TFF enzi za Jamal Malinzi.

The boy, Sugu alikuja akitokea Marekani alikokuwa akiishi na ni Alfred ndo aliniambia ana ahadi naye, nikamuomba twende pamoja.

Nikaiteka shoo, Sugu akawa amevutiwa na mimi na nikamualika ofinisi kwetu kwa mawasiliano zaidi.

Kuanzia siku ile, tukawa wana. Tukiwasiliana kila siku, tukionana mara kwa mara. Ukiniuliza leo hii, msanii ambaye nilitumia naye muda mwingi miongoni mwa wasanii wakubwa na maarufu enzi hizo, ni yeye.

You know why? Kulikuwa na faida nyingi zaidi ya vinywaji mezani kila siku. Sugu ni miongoni mwa wasanii wengi wakubwa wa Bongo Fleva niliokutana na kufanya nao mahojiano, lakini ukiniambia niwapange kwa namba, he will top them.

Anajua mambo mengi. As a journalist, niliongeza sana ufahamu kwa kuongea naye. Anajua siasa in deep, michezo to the maximum, burudani kwa sana, ndondi, dansi, maisha mazuri, maisha ya kifukara, anajua uswahili wetu na kila idara. Kwa kifupi, ukiwa naye, ongea hoja uliyonayo na utashangazwa na mchango wake.

Back to music. Miaka ile, anapambana kuwafanya wasanii wawe na hela nyingi afu wenzake wanamshangaa! Mwaka 2003 aliandaa kitu kinaitwa Hip Hop Summit, katika ukumbi wa WaterFront, Dar es Salaam.

Amini usiamini, wasanii wakubwa wote wa zama zake hawakuwepo ukumbini isipokuwa The Comando Herself, Lady Jay Dee.

Na ilikuwa ni concert iliyolenga wasanii kujitambua. Unajua kwa nini hawakufika? Kwa sababu Too Proud alikuwa na bifu na The Boss, marehemu Ruge Mutahaba.

Wasanii wakaogopa kuhudhuria kwa vile walifikiri ikitambulika walikuwepo, means wanamuunga mlono mbunge huyo wa zamani wa Mbeya mjini, kitu ambacho kitawa cost, maana Clouds Fm, was the only redio inayopiga nyimbo zao kwa ukubwa.

Ajabu sasa, wakati wasanii wakigwaya kuhudhuria, Gadna G. Habash, mtangazaji staa wa Clouds, alikuwa ndiye MC!

Sugu aliniambia enzi hizo, muziki ni utajiri. Mwanzo sikuwa namuelewa, ila kadiri tulivyokuwa tukiongea, siyo tu nilimuelewa, bali nikawalaumu walio katika mamlaka, why hawafanyii kazi mawazo chanya ya Sugu.

The boy, ambaye jina lake la nyumbani anaitwa Mei, sababu ya kuzaliwa mwezi hup, alinipa mifano ya wanamuziki wa Marekani jinsi walivyopata utajiri, kwa kutumia vipaji vyao, akitolea mfano wa mentor wake, Jay Z.

Sugu alisema enzi hizo za miaka ya 2000, kama serikali, kutokana na teknolojia kuwa duni, ingetumia hata tu mtandao wa Posta na Simu, wasanii wangeweza kuuza albamu zao na kupata fedha nyingi.

Let me remind you. Enzi zile wasanii waliuza albamu zao kwa Mhindi mmoja hivi akiitwa Mamuu Store, pale Kariakoo, duka lake likitazamana na kituo cha polisi cha Msimbazi. Kila nakala ya albam, msanii alipewa shilingi mia mbili(200)!

Wakienda pale wanakubaliana, labda tutagonga nakala 200, kwa hiyo msanii anachkua elfu 40 kwa albam. Lakini nani anajua kama zitatoka nakala hizo? 

Enzi hizo wasanii kama Sugu mwenyewe, profesa Jay, Juma Nature, Inspekta Haroun, Mabaga Fresh,  Kwanza Unit na wengineo wakiwa na mashabiki kama wote.

Alichoamini Sugu, kama wangesaidiwa kutumia mtandao kama ws posta, ambao umeenea nchi nzima, mashabiki hata wa vijijini kama kwetu mkumbi, wangenunua albam zao kwa wingi na hivyo kuwapa kipato kikubwa.

Miaka hiyo, Sugu alisema kwa kupata fedha nyingi, wasanii wangewekeza na kutoa ajira kwa watanzania wengine.

Watu walioukamata muziki enzi hizo, wakawa wanamuona chizi, wasanii wenzake wakamuona chizi, serikali ikawa haimuelewi!

Angalia leo, Diamond Platnums ni bilionea, kwa sababu ya utandawazi. Anauza kazi zake mitandaoni, anatangaza na kampuni mbalimbali, anaaminika.

Na siyo yeye tu, wasanii wote wa sasa wana pesa chafu na hili halijaja kwa sababu ya juhudi za walioshika muziki wala serikali, bali teknolojia inawapa wanachostahili.

Miaka ile nilikuwa nashangaa, inakuaje marehemu Elvis Presley anaongoza kwa kupata pesa miongoni mwa wasanii waliofariki? Kumbe ni kwa kazi zao kuendelea kuvutia mashabiki mtandaoni, kitu ambacho kinatupa picha kuwa wanaomsubiri Diamond afilisike, watatangulia wakimuacha akiingiza fedha.

Tunaweza kumdharau mtu kama mtu, lakini hata kama haumpendi, fanyia kazi mawazo yake. Sugu is a Living Legend!


No comments