MWALIMU AKAMATWA KWA KUISHI KINYUMBA NA MWANAFUNZI
 
MWALIMU wa Shule ya Msingi Itete
kata ya Kirando Wilayani Nkasi, Clarence Mwanakurya (29) amekamatwa na Polisi
kwa tuhuma za kumuoa Mwanafunzi wa kidato cha kwanza Jesca Mwanji (20) tangu
mwaka jana na kuishi nae katika majengo ya Serikali yaliyopo katika Shule ya
Msingi Itete anaposoma Mwanafunzi huyo.
Haya yamebainika baada ya Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Peter
Lijuakali kuanza oparesheni ya kuzuia na kupambana na mimba za utotoni ambapo
amewataka Walimu wa Msingi na Sekondari kuziheshimu sketi za shule kwani
zitawaletea matatizo katika kazi zao na maisha kwa ujumla, oparesheni hiyo
imeanza tarehe 01.11.2021 itaendelea mpaka wabainike waliowaachisha Shule
Wanafunzi na kuwaoa.
Sambamba na tukio hilo, pia Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo naye
amekamatwa pamoja na Clarence, sababu ya Mwalimu Mkuu kukamatwa ni kukaa kwake
kimya na kuruhusu Clarence kuishi kuishi na Mwanafunzi huyo.

Post a Comment