HARUNA NIYONZIMA AINGIA FIFA'S CENTURY CLUB

NAHODHA wa
timu ya taifa ya Rwanda, Haruna Niyonzima ameingia kwenye kumbukumbu za FIFA
baada ya kuinga kwenye “FIFA’s Century Club” amabayo inawahusisha wachezaji
waliocheza michezo 100 ya timu za taifa.
Niyonzima
alianza kuichezea timu yake ya taifa ya wakubwa mwaka 2006 na amefanikiwa
kucheza michezo 104 na kufunga magoli 6 na kuwa mchezaji pekee aliyecheza
michezo mingi kwenye timu ya taifa ya Rwanda.
Wachezaji
ambao wanaingia kwenye FIFA’s Century Club ni wachezaji waliocheza michezo ya
kombe la dunia, hatua ya mtoano, michezo ya kufuzu, kombe la mabara na fainali
za Olimpiki kuanzia mwaka 1948 kwa waliocheza timu za wakubwa tu.
Mpaka tarehe
16 Oktoba 2021 ni wachezaji 575 ambao wamefikisha michezo 100 ya huku kimataifa
wakiwa na timu zao kulingana na nakala iliyotolewa na FIFA ya, Rec. Sport
Soccer Statistics Foundation (RSSSF).
Katika jarida
la RSSSF linamtambua Billy Wright kuwa ndie mchezaji wa kwanza kufikisha
michezo 100 ya kimataifa akiwa na timu ya Uingereza mwaka 1959 akimaliza na
michezo 105 wakati mchezaji aliyecheza michezo mingi ni s Bader Al-Mutawa wa
kuwait akiwa na michezo 186.
Credit
Facebook

Post a Comment