WAZIRI MKUU AKATAA TAASISI ZA NIDA, RITA KUUNGANISHWA

 Simba yatikisa hotuba ya Waziri Mkuu Majaliwa - Mwanaspoti


WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, amesema serikali haiwezi kuunganisha taasisi za Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) kutokana na tofauti za majukumu yake. 

Waziri mkuu alisema hayo jana Bungeni mjini Dodoma, akijibu swali la Abubakari Damian Asenga, mbunge wa Kilombero ambaye alishauri taasisi hizo ziunganishwe ili kurahisisha upatikanaji wa vitambulisho vya Taifa ambavyo alisema kwa sasa vinacheleweshwa sana.

Alisema kuwa sababu kubwa inayosababisha kuchelewa kutolewa vitambulisho vya Taifa kwenye mikoa ya pembezoni ni kujiridhisha kwa mtu anayeomba kama ni mtanzania au sio mtanzania.

"nataka niwahakikishie yeyote mtanzania mwenye baba na mama mtanzania atapata kitambulisho "amesema Mhe. Kassim Majaliwa 

No comments