MWENGE WA UHURU WABARIKI BILIONI 11 MTWARA, WAINGIA RUVUMA
MWENGE wa Uhuru ambao umekuwa
ukikimbizwa kila mwaka, umemaliza kazi katika Mkoa wa Mtwara ambako ulizindua
jumla ya miradi 42, yenye thamani ya shilingi bilioni 11 na sasa umeingia mkoani
Ruvuma.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brigedia Jenerali Marco Gaguti
amekabidhi mwenge huo kwa mwenzake wa Ruvuma Brigedia Jenerali Balozi Wilbart
Mbuge katika kijiji cha Sauti moja wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.
Brigedia Gaguti amesema ukiwa mkoani Mtwara mwenge uliweka
mawe ya
msingi, kuzindua, kuona na kukagua jumla ya miradi 42 yenye
thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 11.
Brigedia Jenerali Gaguti amesema ukiwa mkoani humo mwenge wa
uhuru umekimbizwa katika wilaya tano na kupita katika urefu wa kilometa 556.
Brigedia Jenerali Gaguti amesema miradi hiyo imetekelezwa na
serikali kwa kushirikiana na nguvu za wananchi.
Amesema miradi ambayo imebainika kuwa na kasoro atakaa na watendaji
wake ili kufanya marekebisho na kuhakikisha miradi hiyo inatoa huduma bora kwa
wananchi.

Post a Comment