MWANA FA APATA AJALI MOROGORO

MSANII mkongwe wa Hip Hop ambaye
pia ni Mbunge wa Jimbo la Muheza kupitia chama tawala, Hamis Mwijuma maarufu
kama Mwana FA, amepata ajali ya gari mkoani Morogoro leo.
Kamanda wa Polisi Morogoro
Fortunatus Musilim amesema Mbunge huyo yupo salama.
“Nimepata hiyo taarifa, nimetuma
Vijana wangu huko kupata Habari kamili, Mheshimiwa yupo salama lakini kuna
wachache wamepata mshtuko na hata Gari yake ndiyo imetumika kuwapeleka baadhi
yao Hospitali” ——— RPC Musilim.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine
Shigela amesema walionusurika kwenye ajali hiyo ni Watu watano na walipopatia
ajali ni Kingolwira Manispaa ya Morogoro.

Post a Comment