POLISI WADAIWA KUUANA WAKIGOMBEA SITI

KUNA madai kuwa askari wawili wa kitengo cha kupambana na madawa ya kulevya wilayani Mwanga walizusha ugomvi uliopelekea mmoja wao kumpiga risasi mwenzake kisa ikiwa ni kugombea kiti cha mbele ya gari walilokuwa wakilitumia.
Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa, wakiwemo wanakijiji wa kijiji cha Kituri, tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Mei 31, mwaka huu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Amon Kakwale alisema hawezi
kulizungumzia kwa sasa kwa kuwa wako kwenye uchunguzi na wakikamilisha
atalizungumzia kwa kina.
Akisimulia ilivyokuwa, Mwenyekiti wa kijiji cha Kituri wilayani Mwanga, Thomas
Mgala alisema siku hiyo polisi walifika kijijini hapo kuwasaka wauzaji na
watumiaji wa dawa za kulevya.
Mgala alisema wakati polisi hao wawili wakiondoka eneo hilo wakiwa na wenzao,
kuliibuka mzozo kati yao kuhusu nani anatakiwa kukaa siti ya mbele kwenye gari
walilokuwa wakitumia.

Post a Comment