MAMA SAMIA, TEMBELEA PPRA KUNA MADUDU


Employment Opportunity for the Position of the Chief Executive Officer of  the Public Procurement Regulatory Authority (PPRA) - The PPRA Website

 WAFANYABIASHARA, wakitambua dhamira njema ya Rais Samia Suluhu Hassan, wamemuomba atembelee PPRA ili ajionee madudu yanayoendelea ili mradi kuwakwamisha wao kufanya majukumu yao.

Mmoja wa wafanyabiashara hao amelaumu mfumo wa tenda za serikali (TanePs), kwamba una lengo la kuwakwamisha, kwani leo ikiwa ni siku ya mwisho ya kuomba tenda za ICT equipments Supply, mfumo hio tangu asubuhi hauko sawa.

Lakini pia, baadhi ya watumiaji wa TanePs account zao za kuombea hizo tenda zimekuwa blocked kutokana na kujaribu ku-log in mara nyingi. Bila huruma wafanyakazi wa PPRA wamekuwa na majibu ya dharau na kutokuwa na msaada. 

Leo licha ya kutokea changamoto hii, mtu wa idara ya IT hapo PPRA ametoka ofisini makao makuu kabla ya muda na kurudi nyumbani kwake kabla ya muda wa kazi huku akiacha mamia ya Wafanyabiashara wasijuenini cha kufanya.

"Hii nchi ina watu wanaikwamisha kwa makusudi, naiomba serikali ifuatilie PPRA Kuna madudu mengi sana. Inakuaje kila mwaka mfumo unakuwa unasumbua? Kama watu wameshindwa kazi mbona Kuna mamilion ya vijana wazuri mitaani wanaweza kufanya hiyo kazi kwa ufasaha zaidi. Yaani taasisi ya umma inaendeshwa kama genge?, amelalama mfanyabiashara huyo. 

"Hatuwezi kukubali hii ni nchi yetu sote. Mama Samia tembela hapo PPRA uwaulize kwa nini mifumo yao inasumbua kila siku na kwanini hawataki kufungulia watu account zao zilizokuwa blocked."

No comments