ALLY MAYAI AKATWA KUGOMBEA UJUMBE TFF

NAHODHA wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars, Ally Mayai Tembele, amekatwa katika nafasi ya kuwania Ujumbe wa Shirikisho la Soka Nchini, TFF kupitia Chama cha wanasoka, maarufu kama Sputanza.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, Mayai ambaye alitamba na kikosi cha CDA ya Dodoma na Yanga amekosa nafasi hiyo kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kukosa vigezo. Aliyepitishwa kuwania nafasi hiyo kupitia Sputanza ni Abeid Mziba, nyota mwingine wa zamani wa Yanga na Taifa Stars.
Mayai ambaye amejipatia pia umaarufu mkubwa kutokana na uchambuzi wake mahiri wa soka kupitia kituo cha televisheni ya Azam, alikuwa akishikilia nafasi hiyo kwa muda wa miaka minne iliyopita.
Pia Mayai, katika uchaguzi
uliopita aliwania nafasi ya Urais na kushindwa na Wallace Karia.

Post a Comment