WARAKA WA WAZI WA ZIDANE BAADA YA KUONDOKA REAL MADRID


Zinedine Zidane rejects reports he has told Real Madrid players he is  leaving | Sports News,The Indian Express

GWIJI wa soka wa Real Madrid, Zinadine Zidane Zizzou ambaye hii ni mara yake ya pili kujiondoa katika timu hiyo aliyoichezea kwa mafanikio makubwa, ametoa waraka kuelezea nini hasa kimemuondoa klabuni Santiago Bernabeu:


"Nimeamua kuondoka ndani ya Real Madrid kutokana na ukweli kwamba uongozi hauna tena imani kwangu.

"Mara zote kupitia vyombo vya habari utasikia vitisho kuwa nisiposhinda mchezo nitafutwa kazi, nayasikia hayo na hata jumbe za siri za viongozi zinavuja kwenda kwa wanahabari.

"Bahati nzuri kila jambo likitokea wachezaji wangu walikuwa upande wangu na walifanya kila kitu uwanjani kwa ajili yangu, kwa kuwa wananiamini nami nawaamini.

"Sisemi kuwa mimi ni bora sana bali napopewa kazi nafanya kile nilichotumwa kwa nguvu yangu na uwezo wangu na mara zote nimetimiza."


No comments