BENNI McCARTHY AULA BAFANA BAFANA
MSHAMBULIAJI nyota wa zamani wa timu ya Taifa ya Afrika Kusini 'Bafanabafana', Benni McCarthy, ameula baada ya Chama Cha Soka cha Afrika Kusini kumpa mikoba ya kuifundisha timu ya taifa.
McCarthy ambaye kwa sasa ni kocha wa timu ya Amazulu inayoshiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini, ataianza kazi hiyo Mei 29 mwaka huu atakapoiandaa timu hiyo kwa mchezo dhidi ya Zimbabwe.
Mfungaji huyo bora wa muda wote wa
Bafana Bafana akiwa na mabao 31, atasaidiwa na mkongwe mwingine wa timu hiyo, Siyabonga
Nomvethe.

Post a Comment