TPA WASISITIZWA KUACHA MAJUNGU, MAKUNDI
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho, akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kikao cha 29 cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), mara baada ya Waziri huyo kufungua kikao hicho, mkoani Morogoro.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi, Dkt. Leonard Chamuriho, amewataka Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), kuepuka majungu, fitina na makundi katika maeneo ya kazi na badala yake kufanya kazi kwa kushirikiana ili kuleta ufanisi na tija kwa Mamlaka hiyo na Taifa kwa ujumla.
Akizungumza katika Kikao
cha 29 cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Mamlaka hiyo, kilichofanyika mkoani Morogoro,
Waziri huyo amewasisitiza Wafanyakazi hao kushirikiana katika kupinga vitendo vya
wizi na rushwa kwa kufanyakazi kwa weledi na bidii pamoja na kulinda kwa nguvu zote
mahusiano mema baina yao.
“Ni imani yangu kwamba katika kutekeleza majukumu yenu
mliyopewa na Serikali, mtaendeleza utaratibu wa kushirikiana kati ya Menejimenti
na chama chenu cha Wafanyakazi (DOWUTA), kulinda maslahi ya Taifa ndani ya Bandari,
kwa kupinga vitendo vya rushwa na wizi”, amesema Chamuriho.
Ameongeza kuwa, kila mmoja anatakiwa kuheshimu nafasi
ya kila mtu katika eneo la kazi kwani majukumu yao yanategemea na katika kufikia
malengo ya Mamlaka hiyo.
Amewasisitiza wajumbe wa Baraza hilo kutumia kikao hicho,
kupitia kwa makini mpango na bajeti yao, kushaurina hatimae kuja kusimamia utekelezaji
wake.
Ameitaka Menejimenti na wawakilishi wa Chama cha
wafanyakazi cha Mamlaka hiyo, kuwajibika kwa kuhakikisha kuwa
wafanyakazi wote wa Mamlaka wanatambua na kutimiza wajibu wao ipasavyo pamoja na
kusimamia maadili ya utumishi wa umma ili kuongeza ufanisi na tija.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo,
Erick Hamisi, amesema itashirikiana na wafanyakazi wa TPA ili kufikia malengo ya
Taasisi waliyojiwekea.
Kikao hicho cha 29 cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa
TPA kina dhima kuu ya kujadili masuala ya bajeti, utendaji, uendeshaji wa bandari
na utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayofanywa na Mamlaka hiyo.
Imetolewa
na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi

Post a Comment