Mzee Kimiti amsifu Rais Samia kuenzi fikra za Baba wa Taifa

 

MWENYEKITI wa Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Taifa Mh Paul Kimiti ameishukuru Serikali ya Awamu ya sita chini ya Rais wa Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyoenzi fikra na falsafa za Baba wa Taifa kwa kuweza kutenga eneo la kujenga Makumbusho ya Mwalimu Mkoa wa Dodoma.

Kimiti ameyasema hayo katika Maadhimisho ya kitaifa ya kumbukumbu ya miaka 102 ya kuzaliwa kwa Mwl Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika katika Ukumbi wa Mtumba tarehe 13.4.2024 mkoani Dodoma ambapo mgeni rasmi alikuwa Mheshimiwa Dkt Philip Mpango Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wananchi wengi waliojitokeza kushuhudia Maadhimisho ya kumbukumbu hiyo.

Kimiti amesema kuwa jambo hilo litasaidia kutunza Kumbukumbu za Mwasisi huyo wa Taifa kwa kufanya vijana na makundi mengine kwenda kujifunza pia itaongeza pato la Taifa akiamini watu wa mataifa mengi watakuja kujifunza mambo mbalimbali yaliyofanywa na Nyerere.



No comments