TFS kuuza miti aina ya Misaji kielektroniki

 

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) utauza miti aina ya misaji yenye jumla ya meta za ujazo 7,410.001 iliyopo katika Shamba la miti Longuza, Muheza Mkoani Tanga na Shamba la miti Mtibwa lililopo Turiani Mkoani Mororgoro. Jumla ya meta za ujazo 4,647.081 na 2,762.92 zitauzwa katika Shamba la miti Longuza na Mtibwa mtawalia.

 

1.         Miti ya Misaji itauzwa kwa njia ya mnada wa kielektroniki kwa kuzingatia Kanuni ya 31 (ii) ya Kanuni za Misitu za Mwaka 2004. Mnada huu utafanyika siku ya Alhamisi tarehe 14 Machi, 2024 kuanzia saa mbili kamili (02:00) asubuhi hadi saa sita na dakika thelethini na mbili (06:32) mchana kwa Shamba la miti Longuza na Ijumaa tarehe 15 Machi, 2024 kuanzia saa mbili kamili (02:00) asubuhi hadi saa nne na dakika kumi na tano (04:15)  asubuhi kwa Shamba la miti Mtibwa.

1.            Ili kushiriki kwenye mnada, mshiriki atatakiwa kujisajili kupitia anuani ifuatayo http://mis.tfs.go.tz/e-auction kuanzia tarehe ya tangazo hili hadi saa tisa kamili (9:00) mchana siku ya tarehe 12 Machi 2024 siku ya Jumanne. Kwa ajili ya msaada wa usajili, wasiliana na: +255 713 335 926 or +255 766 857 062.

 

2.            Washiriki wanakaribishwa kukagua miti iliyopo shambani wakati wa saa za kazi; kuanzia saa tatu (3:00) asubuhi hadi saa tisa (9:00) alasiri siku za Jumatatu hadi Ijumaa isipokuwa siku za sikukuu. Ukaguzi huo utafanyika kuanzia tarehe ya Tangazo hili hadi tarehe 13 Machi 2024 siku ya Jumatano. Wahifadhi wakuu wa Mashamba husika au wasaidizi wao watakuwepo kwa ajili ya kutoa maelezo ya ziada.

 

Masharti ya kushiriki Mnada huu

 

1.    Mshiriki anapaswa kujisajili na kuthibitisha ushiriki wake kupitia http://mis.tfs.go.tz/e-auction;

 angalau dakika tano (5) ambayo ni saa 01:55 asubuhi kabla ya muda wa mnada kuanza,

 

Muhimu: Uthibitisho baada ya mnada kuanza hautakubaliwa.

 

1.    Malipo yote yafanyike kupitia benki au mitandao ya watoa huduma za kifedha baada ya kupokea hati ya madai (bill) ya Mfumo wa Makusanyo ya Serikali (GePG) itakayopatikana kwenye akaunti ya mshiriki kwenye mfumo wa mnada wa kielektroniki,

 

2.    Mshiriki atakayeshinda atatakiwa kulipa asilimia ishirini na tano (25 %) ya thamani yote ya ununuzi ndani ya siku tatu (3) za kazi baada ya siku ya mnada. Fedha hizo hazitarudishwa endapo mshindi atashindwa kulipia ujazo aliouziwa. Mnunuzi ataruhusiwa kulipia zaidi ya asilimia 25 ya malipo ya kitalu chochote mara tu baada ya kukamilisha malipo ya awali ya 25% kwa vitalu vyote alivyonunua. Asilimia sabini na tano (75 %) iliyobaki italipwa ndani ya siku kumi na nne (14) kuanzia siku ya mnada,

 

3.    Mshiriki atakayefanikiwa kununua miti ya misaji hataruhusiwa kusafirisha   magogo nje ya nchi kwa mujibu wa kanuni ya 50 (1) ya kanuni za misitu za mwaka 2004,


1.    Mshiriki aliyeshinda mnada atatakiwa kuondoa mazao ya misitu aliyonunua ndani ya miezi miwili (siku sitini) baada ya kumaliza kulipa malipo yote kwa asilimia 100. Aidha, endapo kutajitokeza changamoto ambazo zitasababisha kushindwa kuondoa mazao hayo ya misitu kwa muda uliopangwa, barua rasmi iwasilishwe kumjulisha Mhifadhi Mkuu wa Shamba kwa maamuzi,

 

2.    Miti hiyo ya misaji itauzwa mahali ilipo na jinsi ilivyo na mnunuzi hatakuwa na  haki ya kudai fidia baada ya mauzo kufanyika.

 

Wajibu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania;

 

1.    Kupanga ploti za kuuza kama zinavyooneshwa katika Jedwali la orodha ya    bei za kianzio (mrabaha tu) kwa mita moja ya ujazo, na

2.    Kutoa barua za ushindi na hati za madai kwa wanunuzi walioshinda mnada    kwa kila ploti mara baada ya kumalizika kwa mnada.

Ploti za Miti ya Misaji inayouzwa

Ploti zimepangwa kwa mafungu, ambapo kila baada ya masaa mawili na robo(2:15) fungu moja litauzwa. Vilevile ndani ya muda wa mnada uliotengwa kutakuwa na mapumziko (waterbreak) ya dakika mbili kila baada ya fungu moja kuuzwa.

 

Ploti zinazouzwa zimeorodheshwa katika jedwali namba 1 na jedwali namba 2 kama ifuatavyo: -

 

JEDWALI Na. 1; ORODHA YA PLOTI ZITAKAZOUZWA KATIKA SHAMBA LA MITI  LONGUZA SIKU YA ALHAMISI TAREHE 14 MACHI, 2024

 

NA.

JINA LA KIUNGA

UJAZO KWA KILA KIUNGA (M3)

 BEI   PENDEKEZWA (TZS)

FUNGU LITAKALO UZWA

1

KH1-t25

79.719

500,000.00

Fungu Na. 1
 kwa
Masaa 2 na dakika 15

2

KH1-C2

72.711

693,000.00

3

KH1-C3

56.484

693,000.00

4

KH1-C4

65.239

693,000.00

5

KH4-A11

86.756

780,000.00

6

KH4-A13

160.792

780,000.00

7

KH4-A14

100.271

780,000.00

8

KH4-A15

127.224

780,000.00

9

KH4-A16

120.269

780,000.00

10

KH4-A17

185.444

780,000.00

11

KH4-28

109.527

780,000.00

12

KH4-29

165.361

780,000.00

13

KH4-30

145.365

780,000.00

14

KH4-31

161.347

780,000.00

15

KH4-32

75.336

780,000.00

16

KH4-33

151.944

780,000.00

17

KH4-34

121.58

780,000.00

18

KH4-35

47.132

780,000.00

19

KH4-36

71.805

780,000.00

20

KH4-37

137.014

780,000.00

21

KH4-38

81.665

780,000.00

Fungu Na. 2
 kwa
Masaa 2 na dakika 15

22

KH4-39

165.478

780,000.00

23

KH4-40

112.172

780,000.00

24

KH4-41

111.185

780,000.00

25

KH4-42

155.527

780,000.00

26

KH4-43

120.523

780,000.00

27

KH4-44

116.884

780,000.00

28

KH4-45

47.794

780,000.00

29

KH4-46

49.717

780,000.00

30

KH4-47

131.877

780,000.00

31

KH4-48

153.638

780,000.00

32

KH4-49

103.264

780,000.00

33

KH4-50

67.077

780,000.00

34

KH4-51

64.208

780,000.00

35

KH4-52

161.421

780,000.00

36

KH4-53

95.21

780,000.00

37

KH4-54

45.142

780,000.00

38

KH4-55

185.177

780,000.00

39

KH4-56

120.343

780,000.00

40

KH4-57

166.063

780,000.00

41

KH4-58

151.396

780,000.00

 

 JUMLA KUU

4647.081

 

 

 

 

JEDWALI Na. 2: ORODHA YA PLOTI ZITAKAZOUZWA KATIKA SHAMBA LA  MITI MTIBWA SIKU YA IJUMAA TAREHE 15 MACHI, 2024

 

 

 

Na.

JINA LA KIUNGA

UJAZO (M3)

BEI PENDEKEZWA

(Tshs/Cbm)

FUNGU

LITAKALO UZWA

1

LR16A-30

472.621

365,000

 

Masaa 2 na dakika 15

2

LR 16 A-33

462.151

300,000

3

LR 16 A-35

442.266

300,000

4

LR 16 A-37

255.487

180,000

5

LR 16 A-38

260.584

250,000

6

LR 16 A-39

467.758

250,000

7

LR18-9

232.641

600,000

8

LR18-11

169.416

600,000

JUMLA

2,762.92

 

 

 

 

 

Tangazo hili linapatikana katika tovuti zifuatazo za: www.tfs.go.tz na www.mnrt.go.tz

 

 

Limetolewa na Kamishna wa Uhifadhi 

S. L. P. 2228 DODOMA

No comments