Transfoma 87 zaibiwa Dar, Pwani ndani ya muda mfupi

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema mikoa ya Dar es Salaam na Pwani ina changamoto kubwa ya wizi wa transfoma.

Amesema kwa uchache wa transfoma zilizopo bado zinaibwa na kwa kipindi kifupi r tranafoma 87 zimeibwa jambo linalopelekea pale zinapoibwa Wananchi wengi wanatolewa kwenye huduma ya umeme.

Akizungumza Bungeni, Dodoma Dkt. Biteko amewaonya wale wote wanaojihusisha na vitendo vya wizi wa transfoma huku akisema siku zao zinahesabika.

No comments