Katibu UVCCM aja na mpango kamambe wanifaika wa Samia Scholarship


Katibu wa Idara ya Uhusiano wa Kimataifa, Vyuo na Vyuo Vikuu (UVCCM) Taifa *Ndugu Emanuel Martine* mapema leo tarehe 06 Februari, 2024 amekutana na baadhi ya Viongozi wa Matawi ya Vyuo na Vyuo Seneti Mkoa wa Dar Es Salaam tawi la (UDSM Main Campus, Mabibo, Kairuki, DMI, MUHASI, HKMU, CBE) wakiongozwa na Katibu wa Seneti Mkoa wa Dar Es Salaam *Ndugu Mabula M. Mabula* katika Ofisi ndogo za Makao Makuu Upanga, Dar Es Salaam.

Ambapo pia, Viongozi hao waliweza kupata nafasi ya kutembelewa na Mwenyekiti wa Jumuiya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi *Komredi Mohammed Ali Kawaida (MCC)* na Mlezi wa UVCCM vyuo na vyuo vikuu kuwasalimu ambapo pia amewapongeza Viongozi hao kwa kazi nzuri wanazozifanya Vyuoni, na kuwaomba waendelee kukisaidia Chama Cha Mapinduzi katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM Mwaka 2020-2025 huko Vyuoni na amewataka Viongozi wa matawi ya vyuo na vyuo vikuu UVCCM kuwa mstari wa mbele kuisemea serikali vizuri kwani imefanya uwekezaji wa kutosha 

Aidha, Katika kikao hicho ndugu Martine amewapongeza Viongozi hao kwa kazi nzuri wanazoendelea kuzifanya kama viongozi kwenye matawi yao katika kuhakikisha wanakitendea haki Chama Cha Mapinduzi kwa kuendelea kuwapambania na kuwatetea Wanachama wao, pia amewataka kuzitendea haki nafasi zao za kiuongozi katika kutekeleza majukumu yao vizuri na si vinginevyo ili kuendelea kuwa msaada kwa Vijana hao vyuoni.

Vilevile, Ndugu Martine amewaomba Viongozi hao kukutana na Wanufaika wa mkopo wa *Samia ScholarShip* unaomwezesha Mwanafunzi kugharamiwa ada kwa asilimia 100% ya Mkopo, ili kuendelea kuwasikiliza Changamoto zao na kuendelea kuwatia moyo katika masomo yao.

Hata hivyo, Pia ndugu Martine amewataka Viongozi hao kuacha visingizio vya ratiba za masomo na kushindwa kutekeleza majukumu yao kama viongozi na badala yake kuwataka waweze kupangilia ratiba zao vizuri pindi wakiwa vyuoni ili waweze kutekeleza majukumu ya kimasomo pamoja na majukumu ya kiuongozi ili kuzitendea  haki nafasi hizo.

Hali kadharika, Ndugu Martine amesemea Uongozi ni dhamana na badala yake wasitumie kigezo hicho cha uongozi kuvutana vutana au kuoneshana ubavu nani ni bora kuliko mwingine, badala yake washirikiane kwa pamoja ili kukijenga Chama Cha Mapinduzi vyuoni na kuwapigania Wanafunzi vyuoni hapo kwa kusikilizia na kutatua changamoto zao, na kuwaagiza idadi ya Wanachama katika orodha zao kuongezeka na hadi kufikia nusu ya Wanachuo wote vyuoni kujiunga na Chama Cha Mapinduzi.

Mwisho, Ndugu Martine amewataka Viongozi kuendelea kuwajibika kwa hali ya juu ili kutekeleza majukumu yao, ambapo pia amewakaribisha Ofisini viongozi hao na wengine wote, kuwa hakikishia UVCCM  chini ya Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu itaendelea kutoa ushirikiano wakati wote ili kuwasaidia Wanafunzi vyuoni.


Imetolewa na

Idara ya Uhusiano wa Mataifa, Vyuo na Vyuo Vikuu UVCCM Taifa.

No comments