ZMBF kuimarisha Lishe Zanzibar
Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) Mhe.Mama Mariam Mwinyi amesema ZMBF pamoja na Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation kushirikiana na wizara ya afya wamekuja na mradi wa lishe unaolenga kuimarisha lishe kwa watoto umri chini ya miaka 5, wakinamama wajawazito na ustawi wa jamii kiuchumi kwa kuhakikisha utambuzi na matumizi wa mbinu endelevu wa lishe kwa kufadhiliwa na shirika la chakula duniani.
Mama Mariam Mwinyi amesema hayo wakati akifunga wiki ya siku ya lishe ya Kijiji Wilaya ya Kaskazini B, Mkoa wa Kaskazini Unguja tarehe: 19 Januari 2024.
Aidha Mama Mariam Mwinyi ameeleza kuwa mradi huo unatekelezwa Mikoa miwili ya Kaskazini Unguja na Kaskazini Pemba katika Wilaya mbili za Kaskazini B na Wete.
Halikadhalika Mama Mariam Mwinyi amewahimiza wakinamama wajawazito kula chakula bora kuzingatia lishe bora katika makundi sita yenye virutubisho kwa siku moja .
Kwa upande mwingine Mama Mariam Mwinyi ametoa wito kwa wizara ya afya kuandaa mpango rasmi wa utekelezaji wa lishe na afya ya kijiji na kamati ya kitaalamu ya kuratibu shughuli za lishe ngazi ya jamii ili kutokomeza kabisa tatizo la utapiamlo, udumavu, vifo vya wakinamama wajawazito vinavyotokana na lishe duni.

Post a Comment