DC Ifakara, Mkurugenzi wajitokeza kushiriki usafi
Kilombero Leo,
20 Januari, 2024
Kinara wa utunzaji mazingira ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kilombero wakili msomi; Mhe. Dunstan Kyobya akiwa na watumishi, wafanyabiashara na wananchi wa Halmashauri ya Mji Ifakara wakiendelea na kufanya usafi katika maeneo mbalimbali likiwemo eneo la Soko Kuu la Ifakara.
Huu ni utaratibu wa kawaida kwa Kilombero kufanya kusafi wa Mazingira kila mara. Wito wangu kwa wana Kilombero, wana Ifakara na watanzania wote kwa ujumla ni kwamba; ni muhimu kuendelea na desturi ya kufanya usafi wa mazingira katika maeneo yetu tunayoishi na kwenye taasisi wakati wote.
Aidha, kwa kufanya hivi tufanikiwa kuyaweka mazingira yetu safi na kuepuka magonjwa yasiyo ya lazima kama vile kipindupindu n.k
Wakati huo huo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Bi. Zahara Michuzi bega kwa bega na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, watumishi wa Halmashauri, wafanyabiashara na wananchi wa Ifakara katika zoezi la usafi wa mazingira katika maeneo mbalimbali ndani ya Halmashauri yake.
Aidha, Bi. Zahara ameitumia siku hii muhimu kuwaasa wana Ifakara na watanzania wote kwa ujumla kuendelea na kampeni ya kufanya usafi wa mazingira wakati wote badala ya kusubiri siku maalum.
Usafi ni afya, usafi ni uhai. Hivyo, sote tunao wajibu wa kushiriki usafi wa mazingira katika maeneo yetu na maeneo ya taasisi muhimu.
Tanzania imara, 💪 kazi iendelee

Post a Comment