Pwani yafanya sherehe maadhimisho miaka 47 kuzaliwa CCM


Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Pwani leo tarehe *28 - 01 - 2024* kimefanya Sherehe ya uzinduzi wa  maadhimisho ya *Miaka 47* ya Kuzaliwa kwa CCM.

Uzinduzi huo umefanyika  katika *Kata ya Mlanzi,* Wilaya ya Kibiti sambamba na kushiriki kazi za kijamii ikiwemo kukusanya mchanga kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya CCM kata ya Mlanzi,  kufanya usafi katika zahanati ya Mlanzi na  zoezi la usajili wa wanachama kwa njia ya kieletroniki limeendelea.

Aidha uzinduzi huo ulihudhuliwa na Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali ngazi ya Mkoa na Wilaya za Mkoa wa Pwani.

metolewa na:

David Mramba

Katibu wa Siasa na Uenezi CCM

Mkoa wa Pwani.

No comments